Youth Development Organization
Back to News

SHUKRANI KUFUATIA KUKAMILIKA KWA ZOEZI LA USAFI WA FUKWE YA UNUNIO

Events Published on 11 Aug 2026 By YDO Communications Team
SHUKRANI KUFUATIA KUKAMILIKA KWA ZOEZI LA USAFI WA FUKWE YA UNUNIO

Youth Development Organization inapenda kutoa shukrani za dhati na za pekee kwa viongozi wote kwa kuwezesha na kushiriki katika kufanikisha zoezi la usafi wa Fukwe ya Ununio lililofanyika leo.

Tunatambua na kuthamini sana muda, juhudi, ushirikiano na msaada ambao viongozi wameendelea kuutoa katika kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa. Kupitia uongozi na ushirikiano wenu, tumeweza kukamilisha zoezi hili kwa mafanikio na kutoa mchango muhimu katika utunzaji wa mazingira, usafi wa fukwe na uhamasishaji wa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira yetu.

Kwa niaba ya Youth Development Organization, tunawashukuru sana viongozi wetu kwa kuendelea kutuamini, kutuunga mkono na kutuwezesha kutekeleza shughuli zenye manufaa kwa jamii. Mafanikio ya zoezi hili ni matokeo ya ushirikiano, mshikamano na moyo wa kujitolea kutoka kwa kila mmoja wetu.

Tunawaomba tuendelee kushirikiana katika shughuli nyingine za maendeleo na utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya jamii yetu na kizazi kijacho.

Asanteni sana kwa kutuwezesha na kutuunga mkono.

Pamoja Tunaweza Kujenga Mazingira Safi na Jamii Bora.

YOUTH DEVELOPMENT ORGANIZATION
Kwa Maendeleo ya Vijana na Jamii ๐ŸŒฑ

Related Stories