Youth Development Organization tunatoa shukrani za dhati kwa taasisi mbalimbali zilizoungana nasi katika kushiriki chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalum tarehe 24 Agosti 2026.
Tunatoa shukrani za pekee kwa ISHIK Foundation, kwa kuwa Mdhamini Mkuu wa Charity Mwezi na kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha jambo hili lenye kugusa maisha ya watoto na familia zao.
Pia, tunatambua na kuthamini mchango wa taasisi, wadau, wafadhili na watu wote waliojitolea kuungana nasi. Ushirikiano wenu umeleta faraja kubwa kwa watoto na wazazi wao.
Hakika, siku hii ilikuwa ya upendo, umoja na matumaini. Chakula tulichoshiriki pamoja kimerudisha tabasamu kwenye nyuso za watoto na kuwapa wazazi furaha kubwa.
Asanteni sana kwa kuwa sehemu ya sababu ya mtoto kutabasamu. โค๏ธ
Youth Development Organization โ Together We Can Make a Difference. ๐๐คโค๏ธ